Diamond Platnumz
Naogopa
Mapenzi chenga
Yakikupiga unasurrender
Na wengi wakipendwa
Wanasahau kuna kutendwa

Mapenzi chenga
Yakikupiga unasurrender
Na wengi wakipendwa
Wanasahau kuna kutendwa

Wapi mkandarasi wa moyo
Wa ukuta wa mapenzi unadondoka
Kinacho ponza wengi ni moyo
Wakikalia kuti kavu wanadondoka

Wapi mkandarasi wa moyo
Wa ukuta wa mapenzi unadondoka
Kinacho ponza wengi ni moyo
Wakikalia kuti kavu wanadondoka

Unajisifu umempata
Kumbe alo mwacha anamfata
Anachotaka anakipata
Wanasema hawara hana talaka

Unajisifu umempata
Kumbe alo mwacha anamfata
Anachotaka anakipata
Wanasema hawara hana talaka

Naogopa(naogopa)
Naogopa(naogopa)
Naogopa(naogopa)

Kwenye safari ya mapenzi mi nisiyasikee
Naogopa(naogopa)
Naogopa(naogopa)
Naogopa(naogopa)
Tena tochi ya mapenzi isinimulike

Nimeyaona bayana
Ndo maana sitaki kukumbuka ya jana
Alivyonidanganya
Moyo wangu ukapiga danadana
Nimeyaona bayana
Ndo maana sitaki kukumbuka ya jana
Alivyonidanganya moyo wangu ukapiga danadana

Kwani nini za mapendo ila yakaniteka mapenzi
Tena nilimweka moyoni ila akaniona mshenzi
Unaweza sema pesa ndiyo breki ila mapenzi hayasomeki
Umemteka kwa mali na cheki
Kumbe vyombo anakula muuza magazeti
Unayemwita bebi anaweza bebwa kama begi
Mapenzi yanabadilika unaweza ukamwita shemeji
Unayemwita bebi anaweza akabebwa kama begi
Mapenzi yanabadilika unaweza ukamwita shemeji
Unajisifu umempata
Kumbe alo mwacha anamfata
Anachotaka anakipata
Wanasema hawara hana talaka

Unajisifu umempata
Kumbe alo mwacha anamfata
Anachotaka anakipata
Wanasema hawara hana talaka

Naogopa(naogopa)
Naogopa(naogopa)
Naogopa(naogopa)
Kwenye safari ya mapenzi mi nisiyasikee

(naogopa)
Naogopa(naogopa)
Naogopa(naogopa)
Tena tochi ya mapenzi isinimulike