Rayvanny
Penzi
Nawaza kwa nini sikumjuaga zamani, oh mama
Pendo lake zito mpaka lavunja mizani, oh mama
Yeye na mimi kachoo nisharuka nyie oh mama
Wasiojua mapenzi pole jamani
Ati alikuwa bachelor, aibu gani

Aliyeumba dunia akayaumba na mapenzi
Wala hakukosea, ila mwezenu mi siwezi
Nilishapenda ila nikatendwa
Moyo ulidunda maskini roho
Mbona nilikonda licha ya kuhonga
Kuweka viwanda nishaomba poo

Mwenzangu bado hujajua, baki unicheke
Kwako yamechanua, ngoja yanyauke
(Raymond)
Andazi si kitumbua acha mapepe
Ukipendwa tanua kwa nini nisideke?

Jamani nimependa mi, nimependa mi
Nimependa mi nataka nimweke ndani
Mwenzako, nimetendwa mie, nimetendwa mie
Nimetendwa mi, mapenzi siyatamani

Jamani nimependa mi, nimependa mi
Nimependa mi nataka nimweke ndani
Mwenzako, nimetendwa mie, nimetendwa mie
Nimetendwa mi, mapenzi siyatamani
Maana mapenzi ya bara kayachanganya na pwani
Vipi nitajinasua, ameumbika sina budi nisifie
Akipika natamani nilipie, sehemu ya ubaga uliweka kiwembe
Ndio maana mwasi, akaona ajijenge
Wewe kwako sikia, (sikia mwana)
Ila kwako utalia, (utalia sana)
Pili nilikuwaga fundi, fundi zaidi yako