Rayvanny
Nateswa
Hivi nachezea rhumba ama bolingo nangai
Maana nina kiwembe kwenye vita ya masai
Wanitesa mchumba nimependa sishangai
Penzi kitovu uzembe mi nalia we furahi
Ila musiende nyumbani za wageni walete nyumbani kwangu
Chunga taratibu na chaga msije vunja kitanda changu
Nimekunulia na feni msisweti mke wangu
Kama majasho mkimwaga litumie taulo langu

Naaa Baya lako zuri kwangu yote nimekusamehe
Kosa la kwako lawama kwangu acha tu nijitetee
Furaha yako furaha yangu sipendi unyong'onyee
Ukimpenda rafiki yangu sema nikutongezee
Utamu wa pipi ni mate yangu
Wapika na mimi wanakula wenzangu
Ona nakosa siti kwenye gari langu
Kuleni embe acheni kokwa langu

Nateswa nateswa
Mwenzenu nateswa na mapenzi
Jamani nateswa nateswa
Mwenzenu nateswa na mapenzi

Mapenzi anapanga maanani sitaki kuruka kuruka
Sawa ni pande kichwani ukichota itashuka
Niite mfanyakazi wa ndani huna haja kusumbuka
Kwani anakuja muda gani niwatandikie shuka
Siogopi kushare ila usisahau kinga
Japo kwangu fedheha kuku wa chando nashinda
Kweli wanionea nakubali we ndo bingwa
Nipo radhi kulea kama wakikupa mimba
Naaa Baya lako zuri kwangu yote nimekusamehe
Kosa la kwako lawama kwangu acha tu nijitetee
Furaha yako furaha yangu sipendi unyong'onyee
Ukimpenda rafiki yangu sema nikutongezee
Utamu wa pipi ni mate yangu
Wapika na mimi wanakula wenzangu
Ona nakosa siti kwenye gari langu
Kuleni embe acheni kokwa langu

Nateswa nateswa
Mwenzenu nateswa na mapenzi
Jamani nateswa nateswa
Mwenzenu nateswa na mapenzi