Rayvanny
Ni Mungu

[Verse 1 : Rayvanny]
Mindo yule walosema sitofika popote
Ila Mungu akakataa
Mindo yule walonidharau ntakufa kapuku
Nimepata wanashangaa
Mindo yule kipenzi cha Mungu
Wakinichafua ndo kwanza nyota inang'aa
Mindo yule dhahabu kwa majivu
Sasa ukijichanganya usije dhani ni mkaa

[Bridge : Rayvanny]
Mmhh, huuuuuuuh uuh
Huuuuuh uuh, huuuuh uuh
Mungu ananipenda sana
Huuuuuh uuh, huuuuh uuh
Huuuuuh uuuh, huuuuuh
Mungu ananipenda sana

[Chorus : Rayvanny]
Umeona kagari, huyo ni Mungu
Umeona na nyumba, huyo ni Mungu
Ukiona nnaringa, ujue ni Mungu
Afya tele ninayo, huyo ni Mungu
Do you see my car, oooh baba blessings
Do you see my house, ooh baba blessings
Do you see my family, oooh baba blessings
Afya tele tunayo, ooooh baba blessings
[Verse 2 : Rayvanny]
Mindo yule ambaye sikuaminika na yeyote
Nikateseka kwa mitaa
Mindo yule walonisahau na kuniita msumbufu
Nikatengwa na ndugu na jamaa
Mindo yule kipenzi cha Mungu
Kila wakiziba njia ninapita nashangaa
Mindo yule dhahabu kwa majivu
Sasa ukijichanganya usije dhani ni mkaa

[Bridge: Rayvanny]
Eeh Mungu weeeuweeh
Unaweza kumpa hata walie mbagua
Ukinipa weeeuweeh
Atawakipinga ukitaka inakua

[Chorus: Rayvanny]
Umeona mashamba, huyo ni Mungu
Umeona mifugo, huyo ni Mungu
Ona biashara zinasonga, ujue ni Mungu
Mafanikio yote, huyo ni Mungu
Do you see my car, ooh baba blеssings
Do you see my house, ooh baba blessings
Do you see my family, ooh baba blessings
Afya tеle tunayo, ooh baba blessings
[Verse 3 : Mwamposa]
Kataa kutiwa hofu na watu
Jambo lolote lisikutishie wewe
Sema level yako ibadilike
Na ili level yako ibadilike, number one
Lazima uwe na imani
Lazima anza kuamini
Acha kusikitika
Acha kulia, acha kuuzunika
Acha kukaa chini
Anza kuinuka, nakuamini

Eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh

[Chorus: Rayvanny]
Umeona kagari, huyo ni Mungu
Umeona na nyumba, huyo ni Mungu
Ukiona nnaringa, ujue ni Mungu
Afya tele ninayo, huyo ni Mungu